Thursday, March 20, 2014

TUNDU LISU ALIPUA BUNGE LEA KATIBA LEO

Dodoma. 
Mjumbe wa Kamati ya Kanuni za Bunge Maalumu la Katiba, Tundu Lissu amesema ktendo cha Mwenyekiti wa Bunge la Katiba kubadilisha kanuni kwa kutoa muda zaidi wa kuwasilishwa kwa rasimu ya katiba, kinamkera.
Lissu alisema kitendo kama hicho ndicho kilichomfanya yeye na mjumbe mwenzake, Ismail Jussa kutaka kujiuzulu mara mbili kutokana na kupingana na wajumbe wenzao.
Akizungumza na gazeti hili jana mjini hapa, Lissu alisema walitaka kujiuzulu kutokana na kuchoshwa na wajumbe kufikia makubaliano ndani ya vikao, lakini wakitoka nje wanarudi na mabadiliko.
"Tulikuwa hatusongi mbele tunafanya uamuzi na kufikia makubalino, lakini wenzetu baadaye wanaenda kujadiliana upya na kuja na mapendekezo tofauti na kuturudisha nyuma," alisema Lissu.
"Baada ya majadiliano yao, mimi na Jussa tuliomba tujiondoe lakini walituomba tusijiuzulu kwa masharti kuwa tunachokubaliana hawataweza kubadilisha."
Alisema kile ambacho kimeanza kutokea sasa ni kitendo cha Mwenyekiti Sitta kubadilisha kanuni ya 47 (a) ya Bunge hilo juu ya Mwenyekiti wa Tume ya Mabadiliko ya Katiba kupewa muda unaofaa kuwasilisha rasimu katika Bunge Maalumu la Katiba.
Lissu, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki (Chadema), alisema pia hata kubadilisha kanuni kwa kupokea kwanza taarifa ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba na baadaye ndipo Rais Jakaya Kikwete azungumze ni jambo wanalolipinga.

Friday, February 21, 2014

WANACHAMA WA KUDUMU FREEMASON KUJULIKANA

SIRI ZA FREEMANSON TANZANIA ZA FICHUKA!
wp.me
Tanzania ina wanachama hai zaidi ya 600 wa kundi la watu wenye imani ya siri ya Freemasons wakiwa wanatokana na watu wa kada mbalimbali wakiwemo
Like · · · 16 hours ago ·

LOWASSA NEEMA YASHUKA TOKA KWA RAIS KIKWETE

SASA KUSAFIRI KWENDA NCHI YOYOTE AFRIKA MASHARIKI BILA KUULIZWA PASSPORT

Default You don’t need passport to travel all over East Africa

You don’t need passport to travel all over East Africa



President Uhuru Kenyatta flanked by Deputy President William Ruto is shown a demonstration of the use of National Identity card for free movement within the East African Countries by Immigration officer Gladys Kang'ethe shortly before departing J.K.I.Airport for an official visit to Uganda. President Kenyatta exited Kenya and entered Uganda using his national identity card as a demonstration that East Africans do not require a passport or visa to travel to the regional states. PHOTO/PSCU

By NATION TEAM

In Summary
  • Many Kenyans, Burundians, Rwandans, Tanzanians and Ugandans are unaware that they do not require visas to travel to each others’ countries.
  • The East African Passport may be used for travel within the community only. It has a six-months multiple entry validity, which is one of the privileges it accords the holder.


President Kenyatta on Wednesday exited Kenya and entered Uganda using his national identity card as a demonstration that East Africans do not require a passport or visa to travel to the regional states.

The Kenya Airways plane carrying President Kenyatta and his entourage left Jomo Kenyatta International Airport shortly before 5pm.

This was meant to promote the movement of people and goods within the East African Community states without a passport or visa.

Many Kenyans, Burundians, Rwandans, Tanzanians and Ugandans are unaware that they do not require visas to travel to each others’ countries.

Although East Africans can use national passports to travel in the region, those without can use their national IDs.

The East African Passport may be used for travel within the community only. It has a six-months multiple entry validity, which is one of the privileges it accords the holder.

Certificates of identity or inter-state passes are issued by local immigration authorities to citizens who cannot be readily issued with a passport in emergency situations to travel across East Africa in place of a passport.

The common market protocol provides for the use of a machine readable national Identity Card for travel within the East African region, but only for citizens of those partner states which have accepted among themselves the use of such.

East African Community, Commerce and Tourism Cabinet Secretary Phylis Kandie said the introduction of a single visa for East Africans will help ease movement of goods and services across borders.

You don̢۪t need passport to travel all over East Africa - News - nation.co.ke

YAMGABE TUMUACHIE MGABE

MUGABE ATIMIZA MIAKA 90 NA HATAKI WATU KUZUNGUMZIA KUHUSU URITHI WA MADARAKA........NA PIA NI SHABIKI MKUBWA WA CHELSEA...............

Habari za leo, Ijumaa leo nasikia tu watu wakisema 'Rusha Roho'...wikendi inanukia cha muhimu tu bora mtu kutahadhari kuhusu afya na usalama wake. Sasa kwa taarifa ya leo Rais Robert Mugabe anafikisha miaka 90 leo, na kuwa rais mkongwe zaidi Afrika..............una ujumbe upi kwa Mugabe wakati akijiandaa kusherehekea miaka yake 90 ?
Like · · · 103728 · 8 minutes ago ·

WANAJESHI WA TANZANIA JIANDAENI NA HILI JAMBO

UGUMU WAMAISHA WAPELEKEA KUISHI CHOONI

HURUMA JAMANI: FAMILIA YAISHI CHOONI BAADA YA PAA LA NYUMBA YAO KUEZULIWA NA UPEPO

 
Aziza Mohamed(55)akiwa na mjukuu wake katika choo ambacho hivi sasa wamekigeuza kuwa makazi baada ya mvua iliyoambatana na upepo mkali kuezua nyumba yake wilayani Hai. 
FAMILIA moja ya watu watatu akiwemo mtoto wa umri wa miaka saba imelazimika kuhamishia makazi chooni baada ya paa la nyumba waliyokuwa wakiishi kuezuliwa na upepo mkali ulioambatana na mvua iliyonyesha wiki iliyopita katika wilaya ya Hai.Familia hiyo ya Aziza Mohamed (55) mwanae wa kiume, Sikujua Aloyce(40) na mjukuu wake wakazi wa kitongoji cha Kijiweni kijiji cha Mijongweni kata ya Machame Weruweru imekuwa ikiishi kwa zaidi ya siku 14 katika choo hicho ambacho paa lake lilisalimika wakati mvua hiyo ikinyesha.

<<USISAHAU KULIKE UKURAS

URAIA WA MGIMWA WAZUA WASIWASI

Thursday, February 20, 2014

BAYERN MUNICH YAIUA ARSENAL 2-0

WANANDOA WAZUA TIBLILI BUNGE LA KATIBA

MUME NA MKE WAZUA BALAA BUNGE LA KATIBA, WATU WAHOJI,Soma upate habari kamili

 







Zanzibar/Dar. Chama cha National League for Democracy (NLD) Zanzibar kimemtaka, Rais Jakaya Kikwete kufuta uteuzi wa wajumbe wa Bunge Maalumu la Katiba kupitia chama hicho kwa madai kuwa walioteuliwa katika chama hicho ni mtu na mkewe na kufanya uteuzi huo kukosa sura ya Muungano.


Tamko hilo limetolewa na Naibu Katibu Mkuu wa NLD - Zanzibar, Khamis Haji Mussa katika taarifa aliyoisambaza kwa vyombo vya habari mjini hapa juzi, kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, Dk Emmanuel Makaidi amewasilisha majina mawili, la kwake na la mkewe, Modesta Ponera kwa ajili ya uteuzi.


Alisema NLD - Zanzibar kilianza kufuatilia taratibu za uwasilishaji wa barua tangu Desemba 27, mwaka jana kwa kumwandikia barua Katibu Mkuu Kiongozi wa SMZ baada ya kupokea maelekezo ya Ikulu ya Tanzania kwamba majina ya Zanzibar yatafanyiwa kazi visiwani na ya Bara yangepelekwa Ikulu Dar es Salaam.


Alisema kwa mujibu wa utaratibu huo, vyama vyote vyenye usajili wa kudumu vilitakiwa kila kimoja kutoa mtu mmoja kutoka Tanzania Bara na mwingine Zanzibar ili kuwa na sura ya kitaifa, lakini Dk Makaidi alikiuka utaratibu huo.


Makaidi ajitetea


Akizungumzia tuhuma hizo, Dk Makaidi alikiri kuwa Ponela ni mke wake, lakini akasema ni mwanachama wa NLD, hivyo ana haki ya kuteuliwa.


Alisema alipeleka majina manne Ikulu na kwamba upande wa Zanzibar ulitakiwa kufanya hivyo kupitia Ikulu ya Zanzibar... “Walifanya uzembe, hawakupeleka majina ya wanachama wa NLD, matokeo yake nikapeleka majina manne, tukapata uwakilishi.”


Alisema mkewe ni mwanachama wa NLD hivyo ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa katika nafasi yoyote kulingana na sifa zake... “Wanalalamika nini hata chama tawala cha CCM, Rais Jakaya Kikwete ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (Nec) na Mkewe Salma pia ni mjumbe wa Nec.”


Alisema Ponela kuwa mkewe hakumfanyi akose haki zake za msingi na kwamba sifa zake na elimu ndivyo vilivyomfanya Rais amteue.


Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Florens Turuka alipoulizwa alisema Ikulu haina taarifa za suala hilo lakini wanaamini vyama vya siasa vilikaa na kupendekeza majina manne na kuyawasilisha Ikulu, ndipo Rais alipoteua wajumbe mawili kati yake.


Mzimu wa posho walitesa Bunge la Katiba Siku mbili baada ya kuanza kwa Bunge hilo, baadhi ya wajumbe wametaka waongewe posho kwa maelezo kuwa kiasi wanachopewa sasa cha Sh300,000 kwa siku hakiwatoshi kutokana na kupanda kwa gharama za maisha Dodoma soma zaidi

WATUHUMIWA WA MAUAJI WAKAMATWA

TAZAMA PICHA WAUAJI WA WANAWAKE BUTIAMA WAKAMATWA



 AFANDE ADAMU AKIMSOTA KIDOLE MMOJA WA WATUHUMIWA WA MAUAJI BUTIAMA
JESHI la polisi mkoani Mara linawashikilia watu wanne wanaodaiwa kufanya tukio la mauaji ya Mwanamke Nyasatu Paul aliyeuawa kwa kunyongwa shingo na kufukiwa kwenye shimo dogo jirani na shamba ambalo alikuwa analima hivi karibuni katika kijiji cha Kigera Etuma wilayani Butiama.

Taarifa iliyotolewa na Kaimu kamanda wa polisi mkoani Mara Claud Kanyorota imesema watu hao waliokamatwa wamekili kuhusika na matukio kadhaa ya mauaji ya Wanawake kutokana na imani za kishirikina.

Amesema kutokana na oparesheni inayoendeshwa na jeshi la polisi kutokana na mauaji hayo walifanikiwa kuwakamata watu hao na kutoa nyavu ambazo walikuwa wakizitumia baada ya kufanya matukio ya mauji ili wapate samaki ikiwa ni imani ya ushirikina.



Amesema oparesheni hiyo itakuwa ya kudumu kuhakikisha matukio ya mauji ya Wanawake yanayotokea wilayani Butiama na maeneo mengine ya mkoa wa Mara yanakomeshwa ili Wanawake waendelee kufanya shughuli zao za kiuchumi bila kuwa na hofo yoyote.


Katika tukio lingine,Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mara amesema Mkuu wa kituo cha Polisi Buhemba wilayani Butiama na askari wenzake wamekamata bunduki aina ya SMG/SAR na risasi 38 baada ya kufanya upekuzi kwenye nyumba ya Bhoke Kamau(37) zilizokuwa zimehifadhiwa kwenye ghala la chakula baada ya kupata taarifa kutoka kwa wananchi. 


Watu wengine waliokamatwa baada ya upekuzi huo ni Mgosi Silvester(34), Mlimi Silvester na Juma Kabondo(52) wote wakiwa ni wakazi wa wilaya hiyo na kwamba watuhumiwa hao wanatarajia kufikishwa Mahakamani muda wowote.


Kanyorota ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa kwa jeshi la polisi pale watakapopata taarifa za uhalifu na wahalifu ili kuweza kuchukua hatua za haraka za kuwakamata ili kuweza kuepusha matukio ya uhalifu ambayo yamekuwa yakitokea mara kwa mara.

BAADAE HABARI ZILIFIKIA BLOG HII NA KUDAI KUWA WATUHUMIWA HAO TAYARI WAMEFIKISHWA MAHAKAMANI NA KUFUNGULIWA MADA KESI NAMBA 4 YA MWAKA 2014


MWANACHUO WA IFM AKUTWA AMEFARIKI

MWANAFUNZI IFM AKUTWA AMEFARIKI CHUMBANI, SOMA KILICHOTOKEA HAPA

Mwanafunzi wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM), Ibrahim Jackson (24), amekutwa akiwa amekufa katika chumba cha kupumzikia kilichopo chuoni hapo bila mwili wake kuwa najeraha lolote.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Marietha Minangi, alisema tukio hilo lilitokea saa 11:30 juzi jioni katika chumba namba 118 jengo namba D kilichopo mtaa wa Shaban Robert.
NIPASHE lilifika IFM na kuzungumza na Mshauri wa Wanafunzi, Emmanuel Mushi, ambaye alisema kuwa marehemu alikuwa anasomea Shahada ya Usimamizi wa Kodi akiwamwaka wa pili.
Alisema marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu kabla hata hajajiunga na IFM.
Alisema juzi jioni marehemu aliomba funguo kwa ajili ya kwenda kupumzika katika chumba kinachotumiwa kulala nawanafunzi kutoka nje ya nchi pindi wanapofika chuoni hapo kwa ajili yamasomo.
“Nyaraka zake zinaonyesha marehemu alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa kwa muda mrefu, hata kabla hajajiunga na chuohiki, kwa hapa chuoni ugonjwa huo ulikuwa unamtokea mara kwa mara,” alisema Mushi.
Aliongeza kuwa mara baada ya kupewa funguo alikwenda kupumzika katika chumba hicho na baadaye alikutwa amefariki huku mwili wake ukiwa umelala kitandani.
Alisema baada ya tukio hilo walitoa taarifa katika kituo cha polisi napolisi walifika katika chumba hicho na kumpeleka Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) kwa uchunguzi zaidi.
Mushi alisema wamewasiliana na wazazi wake waliopo wilaya ya Mbozi Mkoani Mbeya na taratibu za kuusafirisha mwili huo zitafanyika leo.
Mmoja wa marafiki wa karibu wa marehemu, Peter Alphonce, aliliambia NIPASHE kuwa alikuwa na marehemu siku moja kabla ya kifo chake wakicheza mpira na walimaliza kucheza vizuri na kuagana kuelekea hosteli.
“Nilikuwa naye jana (juzi) tukicheza mpira, hadi saa kumi tulipomaliza aliniaga na kuelekea katika MachavaHostel ndiko anakolala,” alisema Alphonce.

Wednesday, February 19, 2014

MIN SKIRT ZAZUA BALAA UGANDA

Thubutu kuvalia 'Mini Skirt' Uganda 19 Februari, 2014 - Saa 08:24 GMT Facebook Twitter Google+ Tuma kwa rafiki yako Chapisha Maandamano ya kkupinga agizo la wanawake kutovalia sketi fupi Rais wa Uganda, Yoweri Museveni, ametia saini sheria mpya inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya kutembea nusu uchi au kuhusika na vitendo vinavyohusisha picha zenye watu uchi. Wanawake pia wamezuiwa kabisa kuvalia sketi fupi sana au 'Mini Skirt' kama zinavyojulikana au blausi ambazo zinaonyesha kifua chao hadharani na kusababisha hisia za kingono . Taarifa zinazohusiana Uganda Sheria hiyo inasema kuwa nguo kama hizo zitakubalika tu ikiwa zinatumika kwa ajili ya mafunzo au wakati wa michezo na hafla za kitamaduni. Akihutubia waandishi wa habari, mjini Kapmala, waziri wa maadili na utawala bora, Reverend Simon Lokodo alisema kuwa Rais Museveni alipitisha sheria hiyo tarehe 6 mwezi huu, miezi mwili bada ya bunge kuipitisha. Kwa mujibu wa sheria hiyo kamati dhidi ya vitendo hivyo itabuniwa ili iweze kutekeleza sheria hiyo kwa kuhakikisha kuwa picha, au video zenye watu uchi zinanaswa na kuharibiwa. Kamati hiyo, itajumuisha watu kutoka katika sekta mbali mbali ikiwemo ya habari na utumbuizaji. Sheria hiyo inasema kuwa mtu yeyote atakayepatikana akijihusisha na vitendo cya watu kuwa uchi, kuvalia nusu uchi , kuona sinema za watu wakiwa uchi au kuchapisha picha za watu walio uchi kwa lengo la kuleta hisia tofauti utachukuliwa hatua kali za kisheria. Waziri alisema kuwa serikali haitaki watu kuvalia nguo zisizo na heshima na kuzua hisia zisizofaa miongoni mwa watu. Watakaopatikana wakivunja sheria na kuvalia visivyo watafungwa hadi miak 10 na wale watakaopatiokana na hatia ya kuhusisha watoto katika biashara ya ngono watafungwa hadi miaka 15.

Tuesday, February 18, 2014

kagame kumchokoza kikwete

Rais wa Rwanda, Paul Kagame aifanyia ukachero Tanzania....Jeuri yake yadaiwa kujengwa na ushirika wake wa kiintelijensia alioupandikiza ndani ya mfumo wa serikali ya Tanzania

BONDIA FRANCIS CHEKA ATAMANI KUACHA SHULE

BONDIA FRANCIS CHEKA AWA MTORO SHULENI,


Bondia Francis ‘SMG’ Cheka, amedaiwa kuingia darasani siku moja tu tangu aliposajiliwa kama mwanafunzi mpya wa Chuo cha St Joseph cha mjini Morogoro Septemba mwaka jana.
Akizungumza na MWANANCHI, mwalimu wa Cheka aitwaye Mkisi amesema Cheka ameomba kuendelea na masomo baada ya kutoonekana darasani kwa miezi kadhaa bila taarifa yoyote, na kubainisha kuwa hawawezi kumruhusu kuingia muhula wa pili.
Cheka alipewa ufadhili wa masomo chuoni hapo mwaka jana mara baada ya kutwaa ubingwa wa dunia wa WBF Agosti 30, baada ya kumpiga Phil Williams wa Marekani katika pambano lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Mkisi amesema kuwa bondia huyo amekosa vipindi kwa muda mrefu hivyo hawezi kuingia muhula mwingine, kwakuwa atakosa vitu vingi hivyo anapaswa kujisajili kama mwanafunzi wa muhula mpya utakaoanza Machi 24.
“Cheka aliingia darasani siku moja na ‘kupotea’ hata hivyo hivi karibuni alikuja na kutuambia anataka kuendelea na shule ingawa hatuwezi kumuendelezea programu yake ya awali,” alisema Mkisi.
Source:Mwananchi

YANGA KUZUILIWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA JULIUS NYERERE

TAZAMA PICHA JINSI WACHEZAJI WA YANGA WALIPOZUILIWA UWANJA WA NDEGE JANA WAKIHISIWA WAMEBEBA MADAWA



  Jana mchana Team ya Yanga Imekiona cha Moto baada ya kuzuiwa uwanja wa Ndege wa JKIA Hapa Dar Wakielekea Comoro Kwa Ajili ya Mchezo wa Marudiano ...Mtoa nyeti Amehabarisha kuwa Walihisiwa wamebeba mzigo ikabidi upitishwe ukaguzi wa nguvu

na kusababisha safari yao kuchelewa kwa muda wa Nusu saa...Hata hivyo msafara huo uliendelea na safari yao vizuri.Kila la heri Young african.

NAPE NAUYE KUTOA MSIMAMO WA CHAMA CHA CCM

KATIBA MPYA: NEC ya CCM yatoa tamko kuwa serikali 2 ndio msimamo wa chama!

Taarifa hiyo imetolewa kupitia katibu wa Itikadi na Uenezi wa CHAMA hicho ndg. Nape Nnauye. Nape ameeleza kuwa watafanyia kazi changamoto za Muungano zinazolalamikiwa ambapo wameandaa hoja za kuziwasilisha katika bunge la katiba.

WALIOBA KUIPIGA CHINI KATIBA MPYA

KAMA MAMBO YANAENDA KOMBO TUHAIRISHE KATIBA

NIMSHUKURU sana Mungu, muumba wa mbingu na ardhi kwa kuweza kutufikisha tena leo, kama alivyofanya jana, juzi na kila siku bila ya sisi kutumia gharama yoyote. Vitendo vyake kwetu ni vya utukufu mkuu, ingawa mara nyingi binadamu tumekuwa tukifanya vitu vingi vya kumkwaza.
Jaji Joseph Sinde Warioba.
Baada ya kusema maneno hayo, naomba sasa niende kwenye hoja yangu ya leo, ambayo kwa hakika ni ya msingi sana kama bado tunataka kujenga taifa lenye mshikamano, uimara na lisilo na mgawanyiko, kwa misingi ya kabila, dini wala rangi.
Wote tunajua kwamba leo, Bunge maalum la Katiba linaanza vikao vyake mjini Dodoma, likiwa na lengo moja tu, kupata katiba bora kabisa ambayo nchi yetu itaifuata kwa ajili ya ustawi wake na wananchi.
Hii ni baada ya kazi kubwa iliyofanywa na Tume ya Marekebisho ya Katiba, iliyoratibu maoni ya wananchi nchi nzima, iliyofanya kazi chini ya Uenyekiti wa Jaji Joseph Sinde Warioba na Makamu wake, Jaji Augustino Ramadhan.
Ingawa kumekuwa na kutokuelewana kwa hapa na pale miongoni mwa wanasiasa kuhusiana na mchakato huo, ni jambo la kushukuru kwamba hadi sasa, tunapoelekea bungeni, tumeweza kuvumiliana na kukubaliana juu ya mambo ya msingi kwenye katiba yetu.
Hata hivyo, wakati tukielekea katika hatua hii kubwa na muhimu zaidi, zipo dalili zinazoonyesha kwamba kutakuwa na mvutano mkubwa miongoni mwa wajumbe juu ya mambo mbalimbali. Kinachotia shaka, ni baadhi ya vitu ambavyo havionyeshi kama wajumbe hao wako makini na ustawi wa nchi yetu au la.
Ni kwa kutambua umuhimu wa kuiweka mbele nchi yetu kabla ya kitu chochote, ningependa kuwashauri wajumbe wetu kutumia zaidi busara katika mijadala yao ili historia iweze kuandikwa, vinginevyo, tunaweza kujikuta tukizalisha katiba ambayo italeta janga kwa taifa badala ya heri kama ilivyo matarajio ya kila mmoja.
Endapo kila mmoja atalazimisha kupita kwa hoja au mawazo yake, basi ni bora tukasitisha mchakato huu, ili tuufanye kwa utaratibu mwingine bora zaidi, mradi tu mwisho wa siku, iwe ni Tanzania ndiyo iliyofaidika na katiba hiyo, badala ya vyama vya siasa au asasi za kiraia zenye wajumbe wake katika bunge hilo.
Ni lazima tuelewe kuwa siyo kila hoja ya kila mjumbe itapitishwa, zipo zitakazoachwa au kuboreshwa. Wajumbe wetu lazima watazame zaidi faida ya hoja kwa taifa badala ya vyama vyao vya siasa au taasisi wanazoziwakilisha.
Kinachoonekana ni kuwa baadhi ya wajumbe hao, kwa kutotambua kwamba umuhimu wa taifa letu kuwekwa mbele, wamekwenda Dodoma wakiwa na katiba yao, kwamba ni kile tu wanachotaka wao ndicho kinachotakiwa kuwemo ndani yake.
Hii siyo sawa. Kama italazimu, ni bora kama watakubaliana katika kutokukubaliana na zoezi hilo likaahirishwa hadi wakati mwingine, mradi tu, lengo linafikiwa. Itakuwa ni kuwasaliti wananchi, kama wajumbe wetu watakubali kulazimisha kupitisha jambo ambalo wanajua wazi kabisa, halina masilahi kwa wananchi na taifa kwa ujumla wake.
Katiba ni jambo nyeti, tusilipeleke ili mradi tu tumefanya, isipokuwa tulifanye kwa weledi na mapenzi makubwa kwa nchi yetu, kwa sababu tunajua kwamba suala hili linatuhusu sisi tuliopo hivi sasa na vizazi vyetu vijavyo. Tusije kutenda jambo ambalo watoto na wajukuu zetu wakaja kutulaumu hapo baadaye.

Tanzania ni bora zaidi kuliko chama chochote cha siasa, kwa sababu tunaweza kupoteza chama chochote tukaunda kingine, lakini tukiipoteza Tanzania, kamwe hatutaweza tena kuipata popote.
Jipu limepasuka, siwezi kuwa adui kwa kusema ukwel

DIEGO MALADONA AKIJIKUMBUSHIA ENZI ZAKE

I HIZI NI PICHA AKIWA NA MASTAA WA MAN UNITED HUKO DUBAI

ULISHAWAHI KUMUONA TENA DIEGO MARADONA? BASI HIZI NI PICHA AKIWA NA MASTAA WA MAN UNITED HUKO DUBAI

Gwiji wa soka ulimwenguni Diego Maradona amewatembelea mastaa wa Manchester United waliopo huko Dubai kwenye mazoezi maalum. Diego amekutana na wachezaji kadhaa wa United na kupiga nao picha akiwemo Van Persie, Juan Mata, Chicharito, Ashley Young, na David De Gea.
1899958_618548621533966_1414483681_n
article-2561115-1B9286F000000578-681_634x834
article-2561115-1B92963200000578-805_634x841
maradona 1maradona 2 copy

HUENDA AKAINUSURU CHADEMA KATIKA JIMBO LA KALENGA

Like · · 5 hours ago ·

JAMAA ACHINJA MKEWE KISA..........

SAMAHANI PICHA INATISHA..UKATILI TABORA..AMCHINJA MKEWE KISA KUNYIMWA UNYUMBA NAYE AJIKATA KOO NA KUNUSURIKA..!

Mkazi wa mmoja wa Nzega, mkoani Tabora, Juma Kiyabo (45) amemchija mke wake, Wande Monera (34), kabla ya mwenyewe kunusurika kifo baada ya kujijeruhi vibaya shingoni katika jaribio la kutaka kujiua.
Tukio hilo limetokea katika kijiji cha Tazengwa saa 7 usiku wa Februari 16 mwaka huu, huku ikielezwa kuwa sababu ya tukio hilo ni kunyimana unyumba mara kwa mara.

Kaimu Kamanda wa Polisi, ambaye pia ni Mratibu Msaidizi mkoani Tabora, John Kauga amethibitisha kutokea kwa tukio hilo.

Kaunga alisema taarifa za awali zinaonyesha kuwa, mtuhumiwa alikuwa akigombana na mkewe mara kwa mara kwa sababu ya kunyimwa unyumba kabla ya kuamua kuchukua hatua hiyo mbaya.

 Kamanda Kaunga alisema kuwa, mtuhumiwa baada ya kufanya unyama huo, naye alijikata koo kwa lengo la kujiua, lakini hata hivyo jaribio lake lilishindikana na sasa yuko chini ya ulinzi wa polisi.

Monday, February 17, 2014

VIGOGO CHADEMA WAANZA KUPOTEANA


Chama Cha Demokrasia na Maendeleo Chadema KIMEPASUKA vipande vipanda na pengine hiki ndicho KIFO cha CDM.

Aliekuwa KATIBU wa Jimbo la UBUNGO Bwana ALLY MAKWILLO na KATIBU kata wa KATA ya MANZESE Bwana DOTTO MHANDO na KATIBU mwenezi Jimbo la UBUNGO wamejiunga na Cuf leo hii.

Pia aliekuwa M/KITI wa Chadema Wilaya ya NACHINGWEA Bwana Jodan Membe na KATIBU wa Wilaya ya TANDAHIMBA wamejiunga na Cuf.

Hoja ya usaliti yazidi kukitafuna chadema Makwillo aeleza mazito yaliyomo ndani ya chadema matumizi mabovu ya pesa ubaguzi,udini ndio tatizo cdm.

Apanga kuzunguka Jimbo zima kueleza UDHAIFU wa J.Mnyika asema mpaka sasa ni mwaka moja tu uliobaki kabla ya uchaguzi Mnyika ametekeleza AHADI zake kwa 10% hivyo hakuna sababu ya kuendelea kumchagua mbunge MUONGO.

MRISHO NGASA ATAMANI KUIMBA ILI AWE MSANII


HAPA NGASSA NA DIAMOND WALIVYOKUTANA NDANI YA NDEGE KATIKA DILI ZAO TOFAUTI.
Mrisho Khalfan Ngassa jana alifunga tena mabao matatu peke yake katika ushindi wa 5-2 wa Yanga dhidi ya wenyeji Komorozine ya Comoro katika mchezo wa marudiano, Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika.
Ngassa ambaye pia alifunga hat trick wakati Yanga inaichapa mabao 7-0 Komorozine katika mchezo wa kwanza Dar es Salaam, ameiambia BIN ZUBEIRY kwamba mabao yake yote hayo amzawadia mwanamuziki rafiki yake kipenzi, Diamond pichani kulia, kwa sababu alimtabiri atafunga idadi hiyo ya mabao kabla ya mechi hiyo.
Ngassa na Diamond ni marafiki walioshibana na wamewahi kufanya tangazo la biashara pamoja

NYUMBA ILIYOJENGWA NJE YA DUNIA YAWA KIVUTIO CHA THAMANI KULIKO CHOCHOTE DUNIANI

TEKNOLOJIA HIZI???????,HIKI NDICHO CHUMBA KILICHOPO NJE YA DUNIA

Image
Pichani ni mafundi wakiendelea kumalizia ujenzi wa chumba hicho.
Sayansi ya Teknolojia ikiwa inaendelea kushika kasi siku hadi siku, chumba hiki maalum kilichojengwa juu ya safu za milima ya Alpine iliyopo Ufaransa kimepata kuwa kivutio kikubwa kwa watalii wanaotokea sehemu mbalimbali Duniani kutokana na staili ya aina yake walivyokitengeneza kwa kutumia  vioo vilivyozunguka kichumba hicho kidogo  hivyo kumuwezesha mtalii kuona kama vile yupo juu ya Dunia.
Image
Unaambiwa sio rahisi kwa mtu mwenye roho nyepesi kuweza kusimama kwenye kichumba hicho kidogo kutokana na kuwa kileleni mwa mlima Alpine takribani  umbali wa  mita 3800 kutoka usawa wa bahari ambapo utengenezaji wake ulichukua takribani muda wa miaka miwili na ada ya kutembelea kwenye kivutio hicho ni kiasi cha Euro 55 ambazo ni sawa na Tsh 80,000 bila chenji.

ZITTO:SITOPOKEA POSHO YA 300,000 KWA SIKU KWENYE BUNGE LA KATIBA

Zitto akilejea barua yake ya 2011 akiwa anaongea na mwandishi wa gazeti la majira amesema hatapokea posho yoyote kwenye hili bunge la katiba. Zitto amesema ametumwa na wanakigoma kuja kuandika katiba wala sio kipokea posho.
Zitto ameongezea kuwa kuwa huu ni wizi kwa wananchi yaani mwalimu analipwa kati ya 200000 mpaka 300000 kwa mwezi wakati wabunge wanapokea kwa siku

CHADEMA BADO WAKABILIWA NA MAGUMU, TAZAMA

ANGALIA PICHA MSAFARA WA MGOMBEA UBUNGE WA CHADEMA KATIKA JIMBO LA KALENGA AZUIWA NA POLISI MKOANI IRINGA

Polisi mkoani Iringa wakiwa  wameuzua msafara  wa mgombea  ubunge jimbo la Kalenga,  Bi Grace Tendega kupitia Chadema kwa madai  hawakuwa na kibali cha kufanya  maandamano  hayo ya magari  hapa  ni eneo la lango la mji Samora ambapo msafara huo  ulikuwa ukitokea maeneo la Ndiuka kuelekea kwa msimamizi wa uchaguzi  ili kuchukua fomu.
Mgombea  ubunge wa  Chadema Kalenga, Grace Tendega baada ya  kuruhusiwa  gari lake kupita 


Hapa  polisi  wakimtazama  mgombea  huyo akipita  mbele yao
 Habari kamili  itakujia  hivi  punde  hapa  endeleo  kutembelea mtandao  huu 
PICHA na MAZIKU MOTTO

Sunday, February 16, 2014

Je wamjua huyu?

BUNGE LA KATIBA KUANZA 18 FEB MWAKA HUU



Ni Mtanzania gani ungependa awe Spika wa Bunge hili?

AZAM FC ROHO MKONONI

Ni kufa na kupona Azam FC nchini msumbiji


Mechi kati ya Azam FC na Ferroviariao ya hapa Beira Msumbijiimepangwa kupigwa kuanzia saa 9 alasiri za hapa Msumbiji sawana saa 10 za nyumbani Afrika Mashariki.
 Jambo lingine muhimu la kufahamu ni kuwa timu imefika hapaJumatano usiku ni Jumamosi tu jua lilitoka na mvua haikunyeshakabisa.
 Lakini leo tangu alfajiri mvua kubwa imekuwa ikinyesha na angalimetanda mawingu mazitodalili kuwa mvua itaendelea kunyeshakwa muda mrefu kutwa ya leo.
 Kwa muda wote Azam imekuwa ikifanya mazoezi katika viwanjavilivyojaa maji. Mara ya mwisho kufanya mazoezi katika uwanjautakaotumika kwa mchezo leo ilikuwa Ijumaa alasiri na sehemukubwa ya uwanja ilikuwa imejaa maji.

  
 Kwa mujibu wa Kanuni za CAF (Shirikisho la Mpira wa MiguuAfrikazinazoendesha mashindano ya Kombe la Shirikisho,mchezo wowote ambao haukumalizika kutokana na hali mbaya yauwanja (pitch) au hali mbaya ya hewautachezwa ndani ya saa 24baadaye.
  
 Kanuni ya 7(7)inasomeka "Ikiwa mchezo utasitishwa kabla yamuda wa mchezo kumalizika kwa sababu zilizo nje ya uwezohususan kwa sababu ya hali mbaya ya uwanja na/au hali mbayaya hewa kwa uamuzi wa mwamuzimchezo huo utachezwa saa 24baadaye katika uwanja uleule na waamuzi walewaleHatua zoteza kinidhamu (kadi za njano na nyekunduzilizochukuliwa wakatiwa mchezo uliovunjika zitabakia kwa mujibu wa Kanuni ya adhabuya CAF".
  
 Suala la mvua na hali ya uwanja lilijitokeza na kujadiliwa wakatiwa kikao cha matayarisho ya mchezo kilichofanyika jana katikaHoteli ya Tivoli hapa Beira.
  
 Kamishna wa mchezo wa leo Charles Kafatia kutoka Malawialiwaambia wawakilishi wa klabu mbili na waamuzi kutoka Zambiawakiongozwa na Wisdom Chewe kuwa iwapo uwanja utaendeleakuwa katika hali isiyoridhisha basi kanuni zitafuatwa namwasiliano kupelekwa CAF.
  
 Kwa mujibu wa ratiba ya kiutawalaKamishna Kafatia akifutanana mwamuzi wa akiba atakwenda uwanjani saa 4 asubuhi hiikukagua masuala muhimu ikiwepo sehemu ya kuchezea nataratibu za kiusalama.
  
  
 OMOG asemaKuvuka raundi ndiyo malengo ya timu yake
  
 Kocha Mkuu wa Azam Joseph Omog amesema timu yake itaingiadimbani kuwakabili wenyeji Jumapili Ferroviario da Beira kwalengo moja tu la kufuzu kwa raundi inayofuatia katika michuanoya Kombe la Shirikisho Barani Afrika.
  
 Omog amesema matayarisho yote yamekwenda sawa katikamuda wa siku tatu ambazo wamekuwa hapa Beira na kubainishakuwa wachezaji wake wote wako katika hali nzuri kwa ajili yamchezo huo muhimu wa marejeano.
  
 “Tumefanya mazoezi kwa siku tatuhatuna matatizo makubwa yakutukwazajambo pekee ambalo si sawa ni hali ya mvua ambayoimesababisha viwanja kujaa majialibainisha Omog.
  
 Huku akitambua changamoto inayoikabili timu yake katikamchezo huu wa marejeano baada ya kupata ushindi wa 1-0 laKipre Tchetche Jumapili iliyopita jijini Dar es Salaam, kocha Omogamesema wanachukua tahadhali zote kimchezo kwa kuwaelekezawachezaji wake wanacheza kwa lengo la kupata magoli na iwapomagoli yatashindikana basi wazuie kwa umoja na kuepukakuruhusu goli langoni mwao.
 “Mpango ni kuhakikisha tunamiliki mpira kuliko wapinzani wetu,tunaponyang’anywa mpira lazima tujitahidi kuurejkesha mpirakwenye miliki yetu mapema iwezekanavyo na hii ni kazi ya timunzima ambayo itatuwezesha kutimiza malengo yetu” alinenamkufunzi huyo bingwa wa kombe la Shirikisho mwaka jana akiwana klabu ya AC Leopards ya Kongo Brazaville.
  
 Kuhusu utelezi uwanjani amabao unaweza kuvuruga mipango yatimu yake Omogo alisema maelekezo kwa wachezaji wakehususan wa safu ya ulinzi ni kuhakiksha hawaruhusu mipirakuzagaa katika eneo laohivyo lazima waihamisha harakakuepusha hatari.
  
 Aliongeza kuwa baada ya kuwaona wapinzani wao katika mchezowa kwanzaamebaini kuwa wanapendelea kutumia mipira mirefu,hivyo amesema hilo ni eneo lingine muhimu ambalo amelitiliamkazo wakati wa mazoezi.
  
 Mwantika Arejea kikosini
  
 David Mwantika ambaye hakucheza mchezo wa kwanza kwakuwa alikuwa akitumikia adhabu ya kadi nyekundu aliyooneshakwenye wa mwaka jna dhidi ya FAR Rabat ya Morocco anarejealeo na mwalimu Omog ameamua kumpanga sehemu ya beki wakulia ili kuimarisha eneo la ulinzi.
  
  
 Kikosi kitakachoanza leo ni Mwadini Ally, Erasto Nyoni, DavidMwantikaAggrey Morris Said Morad, Michael BolouHimid Mao,Salum Abubakar Brian UmonyKipre Tchethche na Mcha Hamis.
  
 Mwalimu Omog anazo bunduki zake nyingine benchi kamanahodha John Bocco ambaye amerejea kutoka majeruhi na Dar esSalaam aliingia kipindi cha piliPia wapo Jabir Aziz aliyecheza piakipindi cha piliMalika NdeuleIsmael KoneAishi Salum na IbrahiMwaipopo
  
 Watanzania watoa sapoti kubwa
  
 Jumuiya ya Watanzania waishio hapa Msumbiji wakiongozwa naRichard Alloyce wamejipanga vilivyo kuishangilia Azam nawamekuwa wamsaada mkubwa kuelekea mchezo huo.
  
 Kwa mujibu wa kanuni za mashindanodakika 90 zikimalizika bilamshindi kuamuliwaitatumika changamoto ya mikwaju ya penati.Omog amesema timu yake imejiandaa kwa mazingira yote.
Iwapo Azam itafaulu kuitoa Ferroviario itakabiliana na Zesco yaZambia,ikianzia nyumbani kati ya Machi 1 na 2 mwaka huu