Prince Charles na waziri mkuu wa
Uingereza David Cameron ni miongoni mwa wenyeji wa mkutano wa kimataifa
mjini London, wenye lengo la kuzuia uwindaji wa wanyama waliohatarini
kutoweka.
Biashara hiyo yenye kuingiza takriban dola
bilioni 19 kwa mwaka, imeenea kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya
pembe za ndovu nchini China.Zuhura Yunus amezungumza na Rais wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Kikwete kuhusu janga hilo linaloikumba nchi hiyo mwanzo kujua wanakabiliana nalo vipi.
No comments:
Post a Comment