YANGA YAIBUKA NA MAGOLI 12-1
Kwenye
Mechi ya Marudiano ya Raundi ya Awali ya Michuano ya CAF ya CHAMPIONZ
LIGI iliyochezwa Leo huko Uwanja wa Sheikh Said Mohamed International,
Mitsamihuli, Visiwa vya Comoro, Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga,
wameitandika Komorozine de Domoni Bao 5-2 na kutinga Raundi ya Kwanza
kwa Jumla ya Bao 12-2.Wiki iliyopita Jijini Dar es Salaam, Yanga iliichapa Komorozine de Domoni Bao 7-0.
Katika
Mechi ya Leo, Bao za Yanga zilifungwa na Hamis Kiiza, Dakika ya 13,
Simon Msuva, Dakika ya 37, na Bao 3 za Mrisho Ngassa, kwenye Dakika za
22, 87 na 90.
Yanga
sasa imesonga Raundi ya Kwanza ya CAF CHAMPIONZ LIGI ambapo watakutana
na Mabingwa Watetezi, Al Ahly ya Misri, kati ya Februari 28 na Machi 2
na Marudiano kuchezwa kati ya Machi 7 na 9.
KIKOSI CHA YANGA:
Deogratias
Munish "Dida", Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Nadir Haroub "Cannavaro",
Kelvin Yondani, Athuman Idd "Chuji", Simon Msuva, Haruna Niyonzima,
Didier Kavumbagu, Mrisho Ngasa, Hamis Kizza
Akiba: Barthez, Juma Abdul,Luhende, Rajab, Domayo, Dilunga n Bahanuzi
No comments:
Post a Comment